FAQ

  • Kwa sasa huduma zetu zinapatikana mkoa wa Dar es salaam kwenye matawi yaliyoko Mlimani (Mlimani Tower) pamoja na Samora (jengo la CHC) na pia tuna ofisi mikoa ya Morogoro (Morogoro Manispaa, Jengo la NSSF), Mwanza (Kenyata Road,Jengo la PSSSF), Mbeya (Soko Matola jengo la CWT), Arusha(Sekei, jengo la CWT Mkoa), Dodoma (Mtaa wa Jamhuri, jengo la CWT), Rukwa (Jangwani, Jengo la CWT), Mtwara (Jengo la CWT) na Kigoma (Masanga, Jengo la CWT)
  • Wateja pia wanaweza kupata huduma kupitia njia mbadala za huduma za kidigitali za kibenki kama:
  • MwalimuMobile kwa kubofya *150*31#; Ambapo mteja anaweza kuhamisha pesa kwenda mitandao ya simu, kupata taarifa fupi au kulipia bili mbalimbali kama, luku, maji, king’amuzi nk.
  • MwalimuWakala; Huduma hii inampa mteja uwezo wa kuweka na kutoa pesa, kulipa bili za serikali, kubadili pini na kupata taarifa fupi za miamala yake kupitia kwa mawakala wa benki waliosambaa mikoani.
  • MwalimuCard VISA; Card hii inamuwezesha mteja kutoa pesa kupitia ATM nyingi zaidi nchini na nje ya nchi zenye huduma ya VISA. Pia kupitia kadi hii mteja anaweza kufanya manunuzi mtandaoni au kulipia huduma/bidhaa mbalimbali mahali popote penye mashine za malipo (POS)
    • Benki ina ushirika wa kibiashara na Benki ya posta (TPB Bank Plc), mteja wa MCB anaweza kuweka pesa kwenye akaunti yake kupitia tawi lolote la TPB Tanzania
    • Huduma nyingine za Benki ya Mwalimu kama vile kujaza fomu za mikopo, kufungua akaunti na kupata maelezo mbali zinapatikana mikoa yote kupitia ofisi za Chama cha Walimu ngazi ya wilaya.
  • Hapana, Benki ya Mwalimu haiko chini ya Benki ya Posta, inajitegemea. Benki hizi mbili zinashirikiana ambapo huduma ya kuweka pesa katika Benki ya Mwalimu huweza kufanywa kupitia matawi ya benki ya Posta (TPB)
  • Njia pekee ya kufufua akaunti ni kuiwekea fedha. Fedha zinaweza kuwekwa kupitia matawi ya Benki yaliyopo (Dar es Salaam) Mlimani au Samora. Kwa wateja wa mikoani au ambao wako mbali na matawi yetu wanaweza kuweka fedha kupitia Benki ya Posta (TPB) au MwalimuWakala waliopo maeneo mbalimbali nchini.

Unaweza kupata fedha kutoka kwenye akaunti yako kwa njia zifuatazo

  • Kutoa fedha kwa kupitia ATM zote nchini na nje ya nchi zenye huduma ya VISA kwa kutumia MwalimuCard VISA.
  • Kutoa fedha kwa kutumia simu (Mwalimu Mobile) bofya*150*31#
  • Kupitia MwalimuWakala waliopo nchi nzima.
  • Ni rahisi sana, unatakiwa kuandika barua kwa mwajiri (Mkurugenzi wa halmashauri) kuomba kuhamisha mshahara kutoka benki uliyopo kuja Benki ya Mwalimu. Afisa utumishi wa wilaya atabadilisha akaunti kwenye mfumo
  • Ndio Mikutano mikuu ya wanahisa hua inafanyika kila mwaka na taarifa hutolewa kwa wadau wote.
  • Taarifa juu ya mikutano huwa inatolewa kwa njia ya magazeti, akaunti za mitandao ya kijamii ya Benki (Instagram/Facebook/Twitter @mwalimubank), LinkedIn @Mwalimu Commercial Bank, tovuti ya Benki (www.mwalimubank.co.tz) pamoja na ujumbe mfupi kwa njia ya simu kutumwa kwa wanahisa.
  • Mwanahisa anaweza kuuza hisa zake kwa Wakala yeyote aliyeorodheshwa kwenye soko la hisa (DSE), atatakiwa kuwa na kitambulisho pamoja na cheti cha hisa.
  • Ndiyo, unaweza kununua hisa muda wowote kupitia kwa wakala yeyote aliyeorodheshwa kwenye soko la hisa (DSE), utatakiwa kuwa na kitambulisho pamoja na cheti cha hisa.
  • Utapata akaunti yako papo hapo baada ya kukamilisha mahitaji yote ya kufungua akaunti.
  • Ndiyo, ikiwa umestaafu, tunayo fursa kukuwezesha kufungua akaunti na kupitisha mafao ya mkupuo na pensheni ya kila mwezi, pia mstaafu anaweza kukopa.
  • Benki ya Mwalimu ina malengo ya kuwafikia wateja wake kidigitali ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa sasa tuna matawi mawili Dar es salaam na ofisi za kutoa huduma Mikoa ya Mbeya, Mwanza, Morogoro, Arusha, Dodoma, Mtwara, Rukwa na Kigoma. Pia kuna mipango endelevu ya kuongeza ofisi ili kuwafikia wateja kwa urahisi
  • HAPANA, hii sio benki ya walimu pekee, ni benki kwa ajili ya watu wote.
  • Hapana, unaweza kuweka fedha tu kwenye matawi ya Benki ya Posta ila unaweza kutumia ATM zao kutoa fedha kwa kutumia MwalimuCard VISA.
  • Ndiyo, ukiwa na MwalimuCard VISA unaweza kutoa pesa kwenye ATM za CRDB, NMB na benki nyingine nyingi zenye huduma ya VISA ndani na nje ya nchi.
  • Ndiyo, Mwalimu Bank inanunua madeni ya benki nyingine, Bodi ya mikopo na Taasisi nyingine za fedha.
  • Kutokana na kupitishwa kwa kanuni mpya za soko la hisa na hifadhi ya dhamana (DSE-CSD Rules 2022) na Mamlaka ya Masoko ya Mtaji na Dhamana CMSA). Kuanzia tarehe 1 Aprili 2022, CSDR itasitisha utoaji wa Risiti ya Uwekezaji maarufu kama Cheti cha Hisa kwa hisa zote zitakazonunuliwa kwenye soko la Pili (DSE). Badala ya Risiti ya Uwekezaji (Depository Receipt), CSDR itatoa Taarifa ya Akaunti kama uthibitisho wa umiliki wa dhamana kwa mwekezaji. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) inayosema “Taarifa ya Akaunti inayotolewa na CSDR itakua ndio uthibitisho wa umiliki wa dhamana husika”
  • CSDR itaendelea kutuma taarifa ya akaunti moja kwa moja kwa wanahisa kwa barua pepe kila mwisho wa mwezi. Pia tunatoa wito kwa Wanahisa wote kuwasiliana na Mawakala wa Soko la Hisa ili kuhuisha taarifa zao za mawasiliano ikiwemo anuani, namba ya simu na barua pepe ili kuwezesha zoezi la utumaji wa taarifa za akaunti kwa usahihi na kwa wakati.
  • Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Afisa wa benki 0677399921
  • Kikokotoo cha riba ya mkopo kinategemea na gharama za mtaji, amana kutoka kwa wateja, hatari ya mkopo (credit risk margin) na kiasi cha faida (profit margin). Hivyo walimu ambao ni wanahisa wakipitisha mshahara Mwalimu benki na kutumia benki kikamilifu itasaidia kupunguza gharama na kushusha riba.
  • 95% ya wakopaji ni walimu, riba na gharama nafuu, mikopo maalumu kwa wastaafu na waajiriwa wapya.
  • Tumeweza pia kuwafikia walimu na kuwapatia huduma kwa urahisi zaidi kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma, ambapo tulianza na vituo viwili na sasa tuna jumla ya vituo saba. Benki inakaribia kuanza kutoa gawio katika mpango mkakati wa 2021-25
  • Benki imeanza kutengeneza faida kuanzia mwishoni mwa mwaka 2021 pia utoaji wa mikopo umeongezeka ambapo walimu wengi wamenufaika na wanaendelea kunufaika na amana zimeongezeka kutoka kwa wanahisa ambao asilimia kubwa ni walimu.
  • Benki imeweza kuboresha mifumo MwalimuCard VISA, MwalimuMobile na Mawakala Zaidi ya 200 nchi nzima.
  • Mwalimu amewekeza na kuendelea kupata huduma bora na rahisi.
  • Benki inatumia mifumo ya kidigitali, ofisi za mikoa na ofisi za CWT kuwafikia wateja. Njia hii imewezesha walimu nchi nzima kupata huduma za benki kwa urahisi na haraka zaidi.

Wamiliki wa benki ambao ndio wanahisa ni kama wafuatavyo;

  • Walimu waanzilishi                              3%
  • CWT                                                        9%
  • NHIF                                         2%
  • PSSSF                                        2%
  • Umma kwa ujumla                         2%
  • TDCL                                                       2%

Walimu kwa ujumla, CWT na TDCL ni 51.4%

  • Kuna njia mbili za kuweza kuuza au kununua hisa; ya kwanza ni kupitia Aplikesheni ya simu ya Wakala wa soko la hisa (DSE Hisa Kiganjani) na ya pili ni kwa kuandika barua ya kuuza au kununua hisa ukitaja idadi ya hisa, bei ya kuuzia, taarifa za benki ya kufanyia malipo ya hisa hizo pindi zitakapouzwa pamoja na nakala ya kitambulisho cha utaifa. Barua hiyo itatumwa kwa moja ya madalali wa kuuza hisa utakayemchagua kwa ajili ya kukuuzia hisa zako.
  • Mwanahisa anaweza kurithisha au kuhamisha hisa zote au kiasi kwa mtoto au mzazi tu. Atahitajika kuandika barua ya kurithisha au kuhamisha hisa zake akitaja dhumuni au sababu ya kuhamisha, akiambatanisha cheti cha kuzaliwa mtoto na kitambulisho chake kama anahamishia kwa mtoto na kama anahamisha kwa mzazi, mwanahisa ataambatanisha cheti chake cha kuzaliwa pamoja na nakala ya kitambulisho cha mzazi na cha kwake. Barua hiyo itatumwa kwa wakala wa soko la hisa ambaye atajaza fomu maalumu na kufanya uhamisho huo.

HOW CAN WE
HELP YOU?

Contact us at Mwalimu office nearest to you or submit a business inquiry online.